banner

December 28, 2016

NUH MZIWANDA KUJA NA NGOMA HII MPYA AKIWA NA KHADIJA KOPA

NUH MZIWANDA KUJA NA NGOMA HII MPYA AKIWA NA KHADIJA KOPA

Msani Nuh Mziwanda ambaye amefanya vizuri na wimbo wake ‘Jike Shupa’ akiwa na Alikiba amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya mwakani 2017 na kusema kuwa tayari mpaka sasa amejipanga na ngoma kibao kali

Nuh Mziwanda alisema kuwa anatambua kuwa mashabiki zake wanasubiri ngoma mpya lakini kwa mwaka huu hataweza kuachia kazi mpka mwezi wa kwanza ambapo ataachia kazi yake mpya akiwa na Khadja Kopa.
“Kiukweli nina kazi nyingi ndani zote kali lakini mpaka sasa ushindani upo kwenye kazi mbili, kuna kazi moja nimefanya na Khadja Kopa inaitwa ‘Mtaa wa Kongo’ ndiyo nayo tegemea kuachia baada ya Jike Shupa, hiyo kazi nitaachia mwezi wa kwanza kwenye tarehe 20 hivi maana saizi ni kama nimechelewa. Najua kuna watu ambao wanasubiri niaachie ngoma nifeli lakini kiukweli mimi nawaamini sana mashabiki zangu ambao wanasimama na mimi siku zote”. Alisema Nuh Mziwanda kwenye planet bongo ya EA Radio.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search