banner

December 29, 2016

RAIA WA CHINA WASHIKILIWA MAREKANI KWA KOSA LA KUIBA TAARIFA

RAIA WA CHINA WASHIKILIWA MAREKANI KWA KOSA LA KUIBA TAARIFA

Raia watatu wa China wanashtakiwa kwa kosa la kuingia kwenye mifumo ya kompyuta ya Makampuni ya Sheria ya Marekani na kufanya wizi wa mamilioni ya dola katika jiji la New York.
Waendesha mashtaka wanasema kwamba katika kesi hiyo ya msingi kwamba waliweza kupata zaidi ya dola za kimarekani 4 milioni baada ya kupata taarifa za siri kutoka kwenye makampuni hayo ya sheria.
Wanasema walipata faida zaidi baada ya kununua hisa kwenye kampuni hizo za sheria kama sehemu ya wamiliki.
Taarifa zinasema wizi wa kutumia mitandao ya kompyuta unashika kasi kwa nchini nyingi zilizoendelea na kutishia uhai wa biashara nyingi duniani.
Mwanasheria wa kampuni ya Manhattan, Preet Bharara alionya kwamba kesi hiyo ni kelele ya kuwaamsha kutoka usingizi juu ya wizi unaoendelea kwenye mifumo ya kompyuta na mitandao nchini Marekani.
Wachina hao watatu wanashtakiwa kwa kuingia kwenye mawasiliano ya kampuni hizo, kudukua mawasiliano, kufanya miamala ya biashara, na wizi wa mamilioni na kuingia kwenye mifumo ya kompyuta.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search