banner

January 02, 2017

PAPA FRANCIS KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA LA KILUTHERI

PAPA FRANCIS KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA LA KILUTHERI



Papa Francis
Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kivule, Ukonga Dar es Salaam Michael Mgaya (wa pili kushoto) akiwa na wazee wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa ibada. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

                                                                                                     Na Richard Mwaikenda
 

KIONGOZI Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 500 ya kuasisiwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.

Taarifa hiyo imetangazwa jana wakati wa Ibada ya Jumapili ya kuukaribisha mwaka mpya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule Ukonga, Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yatafanyika hivi karibuni eneo ambapo kanisa hilo liliasisiwa nchini Ujerumani ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina zitakazoshuhudiwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.

Kwa hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika Chuo cha Dini cha Makumira, mkoani Arusha, ambapo mnara wa kumbukumbu utajengwa. Kanisa hilo liliasisiwa mwaka 1557.

 
ILI KUSOMA HABARI ZA UHAKIKA KILA SIKU DOWNLOAD APP YETU YA ZOTE KALI BLOG KWENYE SIMU YAKO BONYEZA HAPA NI BUREE

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search