banner

February 28, 2017

MWANARIADHA WA KENYA AFARIKI AKISHIRIKI KILIMANJARO MARATHON JANA

MWANARIADHA WA KENYA AFARIKI AKISHIRIKI KILIMANJARO MARATHON JANA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa masikitiko makubwa anatoa salamu za pole kwa Rais wa Shirikisho la  Riadha  nchini Bw. Anthony Mtaka kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya Bw. Charles Rioba mwenye umri wa miaka 36 aliyefariki  katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika tarehe 26/02/2017  Mkoani Kilimanjaro.
Bw. Rioba alishiriki mbio za Kilometa 21 kwa hiyari, zilizohusisha wananchi wote kwa ujumla wakiwemo viongozi wastaafu zijulikanazo kama ‘run for fun’. Ambapo akiwa katika mbio hizo alianguka na kupatiwa huduma ya kwanza na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na baadae kufariki dunia.
Aidha Mhe. Waziri anatoa pole pia kwa waandaaji wa mashindano hayo na wote ambao wameguswa na msiba huu.
‘Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina la Bwana libarikiwe’.
Imetolewa na
Zawadi Msalla
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
27/02/2017

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search