banner

February 23, 2017

ULIMWENGU KUKIPIGA TIMU MOJA NA NYOTA WA ARSENAL

ULIMWENGU KUKIPIGA TIMU MOJA NA NYOTA WA ARSENAL

Timu ya soka ya AFC Eskilstuna imemsajili nyota wa Zamani wa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Emmanuel Yaw Frimpong kutoka katika klabu moja nchini Urusi.
Eskilstuna wiki chache zilizopita walimsajili nyota wa Tanzania Thomas Ulimwengu ambae alikuwa hana timu baada ya kumalizika kwa mkataba wake na TP Mazembe ya Nchini Kongo.
Frimpong anaungana na Ulimwengu katika kulisongesha Jahazi la timu hiyo ya nchini sweden katika kusaka mafanikio ya ndani ya nchi hiyo na bara la Ulaya kwa Ujumla.
Akizungumza baada ya kujiunga frimpong amesema hii ni nafasi nyingine kwake kung’ara tena na ikiwezekana iwe daraja kwake kurejea nchini uingereza.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search