banner

February 27, 2017

WAJUA KILICHOIUA YANGA TAIFA, HIKI HAPA

WAJUA KILICHOIUA YANGA TAIFA, HIKI HAPA

BEKI wa zamani wa Simba na Yanga na Taifa Stars,  Willy Gari, amesema kipigo cha mabao 2-1 walichokipata Wanajangwani hao kilitokana na wao kushindwa kulinda bao lao la mapema.
Yanga walipata kipigo hicho katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, Gari, alisema wachezaji wa Yanga walionekana kuridhika baada ya Simon Msuva kufunga bao kwa penalti dakika ya tano na beki wa Simba, Novaty Lufunga kumchezea faulo Obrey Chirwa.
Gari kubwa alisema Yanga walikuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na Simba kuwa pungufu uwanjani baada ya beki wao, Janvier Bokungu kutolewa kwa kadi nyekundu.
“Yanga walibweteka na wachezaji  wanapaswa kulaumiwa zaidi katika hili kwani walikuwa wametimia lakini walishindwa  kuibuka na ushindi,” alisema Gari.
Alisema wachezaji wengi wa kikosi cha Yanga hawakuwa fiti kwa asilimia 100,  kwani walionekana kuwa na upungufu mwingi ukiwamo wa kutokaaa na mpira huku viungo wa Simba wakitawala sehemu ya katikati.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search