banner

February 23, 2017

WAKALA WA WAYNE ROONEY AENDA CHINA KUMTAFUTIA TIMU

WAKALA WA WAYNE ROONEY AENDA CHINA KUMTAFUTIA TIMU

Wakala wa Wayne Rooney, Paul Stretford, yupo nchini China kuona kama anaweza kufanya makubaliano ya mshambuliaji huyo kuhamia Ligi Kuu ya China.

Hakuna uhakika wa kufanikisha mpango huo, huku ikionekana kwamba mpango huo hauwezi kufanikishwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Februari 28.

Hata hivyo kutokana na ukweli kuwa Stretford amesafiri kwenda China, inaashiria wazi kuwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho atamruhusu Rooney, 31, kuondoka.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search