banner

February 26, 2017

WINGA SHIZA KICHUYA ANA BAHATI YA KUIFUNGA YANGA

WINGA SHIZA KICHUYA ANA BAHATI YA KUIFUNGA YANGA

Winga Shiza Ramadhani Kichuya amemaliza ukame wa kutofumania nyavu na kuchagiza ushindi wa Simba wa magoli 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi Kuu ya Tanzania bara.

Kichuya sasa anaonekana kuwa na kismati na Yanga, kwani katika mchezo uliopita aliisawazishia Simba goli kwa mkwaju mzuri wa mpira wa kona uliojaa wavuni.

Lakini jana tena aliifanya Simba ifikishe pointi 54 na kuongoza ligi, kwa kutengeneza goli la kusawazisha na kisha baadaye akafunga goli bora kabisa la shuti la mbali.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search