banner

March 30, 2017

AHMAD AHMAD: TUPO NYUMA YA MOROCCO

AHMAD AHMAD: TUPO NYUMA YA MOROCCO

Rais mpya wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Ahmad Ahmad, ameahidi kuiunga mkonoi nchi ya Morocco katika harakati zake za kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026.
Taifa hilo la Afrika kaskazini limewahi kuomba nafasi hiyo zaidi ya mara tatu, lakini lilizidiwa kete na mataifa mengine ambayo yaliwahi kushinda nafasi ya kuwa wenyeji wa fainali hizo kubwa upande wa mchezo wa soka.
Morocco waliwahi kuomba kuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 1994, 1998, 2006 na 2010, lakini walishindwa na nchi za Marekani, Ufaransa, Ujerumani na Afrika kusini.
Ahmad ambaye aliingia madarakani Machi 16 baada ya kumshinda kwa kura aliyekua rais wa CAF Issa Hayatou, amesema kuna ulazima kwa waafrika wote kuungana na kuipa ushirikiano Morocco ili iweze kufanikisha ndoto za kuwa mwenyeji wa fainali za 2026.
“Tumekaa na viongozi wa shirikisho la soka nchini Moroco na tumewashauri kutokata tamaa katika mpango huo, binafsi nimekua wa kwanza kuwaahidi kuwa pamoja nao, na nina uhakika kama tutaendelea kuwa wamoja tutalifanikisha hili kwa ushindi.” Alisema Ahmad
Ahadi ya Ahmad ya kuiunga mkono Morocco, imekuja ikiwa ni siku chache zimepita ambapo rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino alieleza wazi kuwa nchi yoyote ambayo itakua na vigezo vya kutosha hususan upande wa miundo mbinu itakua ya kwanza kufikiriwa kuandaa fainali za 2026.
Afrika kusini inaendelea kuwa nchi pekee ya Afrika kuwahi kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia, baada ya kutimiza ndoto hizo mwaka 2010.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search