banner

March 29, 2017

LIVERPOOL KUMKOSA ADAM LALLANA DHIDI YA EVERTON

LIVERPOOL KUMKOSA ADAM LALLANA DHIDI YA EVERTON

Kiungo wa Liverpool Adam Lallana ataukosa mchezo wa ligi kuu ya England mwishoni mwa juma hili dhidi ya Everton (Merseyside derby), kufuatia jeraha ya paja linalomkabili kwa sasa.
Lallana alipatwa na maumivu ya paja wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Lithuania uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Wembley, ambapo England walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa, Lallana anakadiriwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha mujuma manne.
Hata hivyo jopo la madaktari wa Liverpool lipo katika shughuli ya kumpatia tiba kiungo huyo ili kuangalia uwezekano wa kupunguza muda wa kukaa nje ya uwanja.
Mcheza mwingine wa Liverpool ambaye ana hatihati ya kucheza mchezo dhidi ya Everton mwishoni mwa juma hili, ni nahodha na kiungo Jordan Henderson anaesumbuliwa na maumivu ya mguu, huku kukiwa na taarifa njema za kurejea kwa Philippe Coutinho na Roberto Firmino baada ya kumaliza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Paraguay uliochezwa leo alfajiri.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search