banner

March 08, 2017

MWENYEKITI, KATIBU CHADEMA LINDI WATOKA GEREZANI

MWENYEKITI, KATIBU CHADEMA LINDI WATOKA GEREZANI

Mahakama Kuu imemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Seleman Methew na Katibu wa Tawi wa kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila waliokuwa wakitumikia kifungo cha miezi minane kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali.
Viongozi hao wa Chadema wamekuwa gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana.
Aidha, Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Deusdedit Kamalamo amesema kuwa baada ya mahakama kuwahukumu wateja wake kwenda jela miezi minane na kutoa na kutoa nafasi ya kukata rufaa, walikata rufaa na kukata hati ya dharura kwa ajili ya dhamana.
“Maamuzi haya ambayo yametolewa leo, si jambo geni, aliyefungwa anaweza kufungua hati ya dharura ya kupata dhamana wakati akisubiri dhamana yake,”amesema Kamalamo.
Hata hivyo, kabla ya kutoa uamuzi wa kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2017, Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, alisikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na baadaye kuwaachia huru kwa kuwataka waweke dhamana ya sh. 2 milioni kwa kila mmoja.
Jaji Mlacha amesema kuwa Mahakama imejiridhisha kuwa kesi ya Kupulila na Methew, ambayo itasikilizwa tena Mei 3 mwaka huu inaweza kuendelea wakati wakiwa nje kwa dhamana.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search