banner

April 30, 2017

BAADA YA AZAM KUMLALAMIKIA REFA KIPIGO CHA SIMBA, BOCCO ATOA YAKE YA MOYONI

BAADA YA AZAM KUMLALAMIKIA REFA KIPIGO CHA SIMBA, BOCCO ATOA YAKE YA MOYONI

Mara baada ya Simba kufanikiwa kuifunga Azam FC bao 1-0 na kutinga fainali ya Kombe la FA, wachezaji na baadhi ya memba wao wa benchi la ufundi walionekana wakimlalamikia mwamuzi kuwa hakuwatendea haki katika mchezo wao huo, nahodha wa Azam FC, John Bocco naye amezungumza kuhusu mwamuzi wa mchezo wao.
Simba na Azam FC zilikutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa katika nusu fainali ya Kombe la FA ambapo Simba ilipata ushindi huo kwa bao lililofungwa na Mohamed Ibrahim, hivyo kusubiri fainali dhidi ya Yanga au Mbao FC.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Bocco alisema: Mwamuzi naye ni binaadamu, anaweza kuwa na makosa yake, tunakubali tumepoteza mchezo, kadi nyekundu ilitupunguza kasi lakini tunakubali kwa haki kuwa tumepoteza mchezo," alisema Bocco.
 Katika mchezo huo mwamuzi alimPa kadi nyekundu kiungo wa Azam, Aboubakari Salum 'Sure Boy' katika dakika ya 16 huku Simba nao wakipata pigo dakika ya 76 kwa kumpoteza Mohammed Ibrahim ambaye naye alipewa kadi ya pili ya njano.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search