banner

April 29, 2017

CONTE: HAZARD ANAWEZA KUONDOKA CHELSEA

CONTE: HAZARD ANAWEZA KUONDOKA CHELSEA

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte hana uhakika kama mshambuliaji wake Eden Hazard atakuwepo Darajani msimu ujao.

Hazard mwenye umri wa miaka 26 amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu akifunga mabao 15 na kuisadia Chelsea kusogelea ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza.

Tetesi za Hazard kutakiwa na Real Madrid zimepelekea Conte kuanza kuwa na mashaka kama ataendelea kuwepo Stamford Bridge licha ya kuamini mbelgiji huyo anafurahia maisha ndani ya Stamford Bridge.

Conte alisema hawezi kuzungumza kwa uhakika uwepo wa Hazard msimu ujao kwa kuwa katika mpira mambo hubadilika.

” Nafikiri haiwezekani kwangu kuwajibika kwa hili, sio kwa Eden tu bali kwa kila mchezaji. Katika hali hii, klabu ndio ina maamuzi ya mwisho. Naweza kutoa maoni yangu binafsi lakini klabu ndio yenye kauli ya mwisho. ”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search