banner

April 20, 2017

POINTI TATU ZAKWAMA TENA SIMBA

POINTI TATU ZAKWAMA TENA SIMBA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania, imeshindwa kutoa uamuzi wa pointi tatu za Simba walizopewa baada ya kupokwa Kagera Sugar ambao walimchezesha mchezaji Mohamed Fakhi, aliyedaiwa kuwa na kadi tatu za njano.
Kikao hicho kilishindwa kufanyika jana baada ya suala hilo kuhamishiwa makosa ya mtandaoni (Cybercrime), ili kubaini kama barua pepe (email) ya ripoti ya mwamuzi si ya uongo.
Habari za ndani ambazo BINGWA limezipata zinasema kamati hiyo imepeleka vielelezo vyake (Cybercrime) ili kubaini kama ni kweli ‘email’ iliyotumwa kwenye bodi ya ligi si ya uongo.
“Leo (jana) vielelezo vimepelekwa cybercrime ili kubaini ukweli wa barua pepe ya ripoti ya mwamuzi ambayo awali ilisema Fakhi alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya African Lyon. Ila kuna wajumbe wametoa hoja kwamba huenda ‘email’ hiyo ikawa ya uongo hivyo tumepeleka ili kupata uthibitisho,” kilisema chanzo hicho.
Kagera imeomba kupitiwa upya uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ambayo iliiwanyang’anya pointi tatu na kuwapa Simba ambao waliwasilisha rufaa ya beki Fakhi.
Kamati ya saa 72 iliiadhibu Kagera kwa mujibu wa kanuni ya 3 (37) ambayo ilitoa pointi tatu na magoli matatu kwa Simba, ambao kwenye mchezo huo walifungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Kikao hicho kimekuja baada ya Kagera Sugar kuwasilisha rufaa kuomba marejeo (review) kufuatia kupokwa pointi hizo tatu na Kamati ya Saa 72.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search