banner

April 23, 2017

STORI KUBWA 5 ZA USAJILI : Zidane Aanza Kumnyatia Mbabe wa Messi

STORI KUBWA 5 ZA USAJILI : Zidane Aanza Kumnyatia Mbabe wa Messi

Kiwango cha beki wa Juventus Leonardo Bonucci kwenye mchezo dhidi ya Barcelona akifanikiwa kuwadhibiti wakali Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, kimeibua hisia juu ya kuwa mbadala wa Pepe katika klabu ya Real Madrid.
Kocha Zinedine Zidane ameishauri bodi ya klabu hiyo kumsajili beki huyo kisiki kwani wanaamini akicheza pamoja na Sergio Ramos watatengeneza ukuta imara na kuiboresha zaidi safu ya ulinzi ya klabu hiyo. Pepe anatarajia kuondoka mwishoni wa msimu na hivyo raia huyo wa Italia anatajwa kama mbadala wake.
Real ipo tayari kutoka paundi 60 milioni ikiwa ni zaidi ya dau lililovunja rekodi ya usajili wa beki David Luiz alipotimkia PSG akitokea Chelsea.
GUARDIOLA ATAJWA KUMRITHI ENRIQUE BARCELONA
Kufuatia kocha Luis Enrique kutangaza kuachana na FC Barcelona baada ya kumalizika kwa msimu huu klabu hiyo ipo kwenye mawindo makali ya kusaka mrithi wake.
Barcelona wanahusishwa na makocha mbalimbali barani Ulaya ambao mmoja wao atachukua nafasi ya Mhispania huyo huku kocha wa zamani wa timu hiyo Pep Guardiola akitajwa katika orodha hiyo.
Guardiola ambaye ndio msimu wake wa kwanza na Manchester City hana mpango wa kuondoka klabuni hapo hivi karibuni hivyo Barcelona itabidi iendeleze mazungumzo na Ernesto Valverde, Jorge Sampaoli na Ronaldo Koeman ili mmoja wao awe mrithi wa Enrique.
PSG WATIA MGUU KWA MBAPPE
Wakiwa wapinzani wakubwa wa AS Monaco klabu ya Paris St. Germain imeingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnasa mshambuliaji wao hatari Kylian Mbappe.
Mbappe anahusishwa kuondoka Stade Louis II katika usajili wa majira ya joto huku klabu za Manchester United na Real Madrid zikiwa makini kumfatilia kinda huyo anayekuja kwa kasi.
Rais wa PSG Nasser Al Khelaifi ana mpango wa kumwaga pesa ili kupata saini ya kijana huyo kufuatia kiwango alichokionyesha na kupachika mabao 22 katika michezo 36 msimu huu.
OZIL NJE, TURAN NDANI
Arsenal wameanza kukubalina na hali kwamba Mesut Ozil huenda akawakacha katika majira ya joto hivyo wameamua kumuangukia nyota wa Barcelona Arda Turan kuziba pengo la Mjerumani huyo.
Ozil hajasaini mkataba mpya klabuni hapo na akihitaji matakwa yake yatekelezwe ndio asaini huku Arsenal ikimwekea ngumu kufanya hivyo. Turan nafasi yake katika kikosi cha Barca ni hafifu kutoka na kuwepo idadi kubwa ya viungo wenye uwezo mkubwa ndani ya timu hiyo.
Arsenal wataishawishi Barcelona kwa paundi 25 milioni ili kumnyakua raia huyo wa Uturuki kwenda kuisaidia kufanya vizuri katika michuano mbalimbali.
AC MILAN MPYA YASUKWA

Klabu yavAC Milan huenda ikarejea katika hadhi yake ya miaka ya nyuma kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya wamiliki wapya wakiongozwa na Yonghong Li kumwaga pesa ya usajili ili kuimarisha kikosi hicho.
Milan itaboresha pia uwanja wake kutokana na uwekezaji huo huku ikitumia kitita cha paundi 150 milioni katika kusajili nyota mbalimbali baada ya kumalizika kwa msimu.
Miongoni mwa wachezaji wanaohitajika ni pamoja na Cesc Fabregas, Romelu Lukaku, Karim Benzema, Alvaro Morata na Sead Kolasinac.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search