banner

May 05, 2017

HARUNA NIYONZIMA AAMUA KUZITAJA TP MAZEMBE NA AL AHLY

HARUNA NIYONZIMA AAMUA KUZITAJA TP MAZEMBE NA AL AHLY

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayeichezea Yanga, Haruna Niyonzima, ameushauri uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unasajili wachezaji wenye uwezoefu wa michuano ya kimataifa ili timu hiyo iweze kufikia malengo yao ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Niyonzima amedai Kuwa Yanga ni timu kubwa Afrika hivyo, ilipaswa kubadili aina ya usajili wake kwa wachezaji wazawa na wale wa kimataifa ili kufikia ubora wa klabu kubwa kama TP. Mazembe, Zamalek na Al Ahly.
“Ukiacha msimu uliopita ambao ulikuwa na mafanikio kwetu, huko nyuma, hatukuwa na timu bora na hiyo asilimia kubwa ya wachezaji walikosa uzoefu kwenye michuano ya kimataifa wakiwemo wageni, sasa ili kutimiza ndoto za klabu nilazima uongozi ubadilike na kufanya usajili wa wachezaji wenye uzoefu,” amesema Niyonzima.
Nahodha huyo msaidizi kwenye kikosi cha Yanga na timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ pia alizungumzia mstakabali wake kwa msimu ujao na kudai bado ni mchezaji wa timu hiyo na hajafirikia kuachana na timu hiyo licha ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.
Amesema Yanga ndiyo timu pekee aliyoichezea kwa muda mrefu, na kupata nayo mafanikio makubwa hivyo kwake ni sehemu salama ingawa lolote linaweza kutokea, baada ya msimu huu kuamalizika, lakini hilo hiyo ni mipango ya Mungu anayejua vinavyokuja mbele lakini hakuna ofa yoyote aliyopata hadi sasa.
“Nimekuwa nikisikia kwenye vyombo vya Habari kwamba Niyonzima nimesaini Simba, mara ninaondoka Yanga nakwenda Cyprus, hayo yote ni maneno ya kunichafua na kunigombanisha na uongozi, bado nipo Yanga na sijapata ofa yoyote na Mungu akipenda baada ya ligi kuisha kama uongozi ukiona nafaa kuwa sehemu ya timu yao tunaweza kuzungumza na kufikia muafaka,” amesema.
Niyonzima amejiunga na Yanga, mwaka 2011,  akitokea APR ya Rwanda na ameichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kuisaidia kubeba mataji mawili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, moja la Kagame, Kombe moja la FA, na ngao mbili za Hisani.

CHANZO: GOAL

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search