banner

May 01, 2017

IBRAHIMOVIC AANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA MEMBA WA MAN UNITED ILI KUWAAGA

IBRAHIMOVIC AANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA MEMBA WA MAN UNITED ILI KUWAAGA

Straika mkongwe wa Manchester United,  Zlatan Ibrahimovic amepanga kuwaandalia chakula cha jioni wachezaji na memba wenzake wa timu yake jumla yao wakia ni 50 kuwashukuru kwa kuonyesha kumuunga mkono katika kipindi hiki kigumu alichonacho.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, anatarajia kuwakaribisha wahezaji, makocha, memba wa benchi la ufundi, wauchua misuli na wasaidizi wa karibu wa klabu kwa ajili ya mlo huo ambapo watapata nafasi ya kuzungumza machache.
Imeshaelezwa kuwa mkongwe huyo amekataa kusaini mkataba mpya kwa kuwa anasubiri kuona maendelea ya afya yake kwanza, ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi tisa huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwezi wa sita mwaka huu.
“Ameamua kuwatoa wote kwenda kula, na ninaamini inaweza kuwa ni wakati wake wa kusema kwaheri kwa kipindi ambacho atakuwa nje kwa matibabu,” kilisema chanzo cha habari.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search