banner

May 24, 2017

JUVENTUS YAKAMILISHA USAJILI WA CUADRADO, YAMPA MIAKA MITATU

JUVENTUS YAKAMILISHA USAJILI WA CUADRADO, YAMPA MIAKA MITATU

Timu ya Juventus ya Italia imemsajili winga Juan Cuadrado kwa mkataba wa miaka mitatu, wenye thamani ya pauni milioni 17.
Cuadrado amesajiliwa na Juventus baada ya kucheza hapo kwa msimu miwili kwa mkopo akitokea Klabu ya Chelsea ya nchini England.

Winga huyu ameichezea timu hiyo jumla ya michezo 83, baada ya kushindwa kufanya vizuri na Chelsea ambapo walimsajili kwa kiasi cha pauni million 23.3 akitokea Fiorentina.

Chini ya Kocha Massimiliano Allegri, Cuadrado ametwaa ubingwa wa Seria A mara mbili, Kombe la Copa Italia mara mbili, na kuisaidia timu yake kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Juni 3, mwaka huu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search