banner

May 13, 2017

CHELSEA MABINGWA WAPYA WA PREMIER LEAGUE, KOCHA CONTE APAGAWA WA KWA FURAHA

CHELSEA MABINGWA WAPYA WA PREMIER LEAGUE, KOCHA CONTE APAGAWA WA KWA FURAHA



WEST BROM: Foster; Dawson, McAuley (Wilson, 64), Evans, Nyom, Fletcher, Brunt, Livermore, Field (Yacob, 51), McClean (Chadli, 59), Rondon 
Subs not used: Robson-Kanu, Morrison, Wilson, Myhill, Leko
Booked: McClean, Wilson, Field 
Manager: Tony Pulis


CHELSEA: Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill, Moses (Zouma, 86), Fabregas, Matic, Alonso, Pedro (Batshuayi, 76), Hazard (Willian, 75) Diego Costa
Subs not used: Begovic, Ake, Kante, Terry
Goal: Batshuayi 81
Manager: Antonio Conte
Referee: Michael Oliver
Attendance: 25,367 

Chelsea imetangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ baada ya kuifunga West Bromwich Albion bao 1-0, usiku wa kuamkia leo na kufikisha pointi 87 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika ligi hiyo.

Hiyo inakuja baada ya kuwa na msimu mbaya mwaka jana kiasi cha kusababisha kumfukuza aliyekuwa kocha wao, Jose Mourinho, hatimaye Chelsea imerejea kwa nguvu katika soka la ushindani na kukamilisha kile ambacho ilikifanya kwa muda mrefu msimu huu wa 2016/17.

Bao lililofungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82 liliipa Chelsea ushindi huo na kujihakikishia ubingwa huku kocha wao, Antonio Conte akipagawa kwa furaha na kujikuta akiingia uwanjani akishangilia.

Conte alishangilia kwa staili yake ya kurukaruka na kuingia katika sehemu ya kuchezea, ambapo ilibidi wasaidizi wake na mwamuzi wa akiba kumfuata kumsisitiza kutulia.

Kabla ya kufungwa kwa bao hilo mchezo ulikuwa mgumu na timu zote zilishambuliana kwa zamu huku ikionekana mchezo utamalizika kwa suluhu.

Michy Batshuayi alianzia benchi katika mchezo huo na kuingia katika dakika ya 76 akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez ambaye alishindwa kung’ara.

Ubingwa huo umekuja ikiwa timu hiyo imesaliwa na mechi mbili mkononi, na hivyo kufanya sasa vita iliyosalia ni kwa timu nyingine tano zinazowania kuwemo katika nafasi nne za juu ili kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Totenham inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Premier League ikiwa na pointi 77, ikishinda michezo yote iliyosalia itafikisha pointi 86 ambazo tayari zimeshavukwa na Chelsea ambao wana pointi 87.
 
MABINGWA WALIOPITA
2004–05: Chelsea
2005–06: Chelsea
2006–07: Man United    
2007–08: Man United    
2008–09: Man United
2009–10: Chelsea 
2010–11: Man United 
2011–12: Man City
2012–13: Man United
2013–14: ManCity
2014–15: Chelsea
2015–16: Leicester City
2016-17: Chelsea





















Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search