banner

May 19, 2017

KUELEKEA MECHI ZA MWISHO WA MSIMU, TFF YATOA ANGALIZO, MECHI ZOTE KUANZA SAA 10:00 JIONI

KUELEKEA MECHI ZA MWISHO WA MSIMU, TFF YATOA ANGALIZO, MECHI ZOTE KUANZA SAA 10:00 JIONI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa tamko la kuwafahamisha kuwa mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 zinatakiwa kuanza kuchezwa kuanzia saa 10.00 jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Katika taarifa yake iliyoitoa leo Ijumaa, TFF imeeleza kuwa muda huo umepangwa ili kuhakikisha timu zote zinamaliza mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika muda uliopangwa.

Timu zote zitashuka uwanjani Jumamosi ya Mei 20, mwaka huu kwa muda mmoja ili kuhitimisha ligi hiyo ambayo bingwa anatarajiwa kuwa ni Yanga na lengo kubwa ni kukwepa upangwaji wa matokeo.

TFF imesisitiza kuwa ni jukumu la kila kamishna kuhakikisha mechi anayosimamia inaanza katika muda ulipangwa bila kujali kama kuna mgeni rasmi au la.
Michezo ya Mei 20, 2017
Azam         v    Kagera Sugar    Azam Complex
Majimaji        v    Mbeya City    Majimaji
Simba         v    Mwadui        Taifa
Mbao FC        v    Yanga         Kirumba
Stand United    v    Ruvu Shooting    Kambarage
Mtibwa Sugar    v    Toto African    Manungu
Prison         v    African Lyon    Sokoine
Ndanda FC        v    JKT Ruvu        Nangwanda

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search