banner

May 14, 2017

LIVERPOOL YASHINDA 4-0, MATUMAINI YA ARSENAL YAFIFIA, HULL CITY YASHUKA DARAJA

LIVERPOOL YASHINDA 4-0, MATUMAINI YA ARSENAL YAFIFIA, HULL CITY YASHUKA DARAJA

Matumaini ya Arsenal kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yamefifia baada ya Liverpool kuipa kichapo cha hasira West Ham United mabao 4-0, leo Jumapili.
Kwa matokeo hayo Liverpool imerejea katika nafasi ya tatu ya Premier League ikiwa imesaliwa na mchezo mmoja kabla ya kumaliza ligi, ambapo ina pointi 73 ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 70 ikiwa imesaliwa na michezo miwili.
Arsenal ipo nafasi ya tano kwa kuwa na pointi 69 na kusaliwa michezo miwili, kama Liverpool isingeshinda leo, kisha Arsenal ikashinda michezo yake miwili, ingekuwa na nafasi ya kuingia katika ‘Top Four’.
Pamoja na hivyo nafasi kwa Arsenal bado ipo ikiwa itashinda michezo yake mwili iliyosalia kisha Liverpool ikapoteza mchezo wake wa mwisho au Man City nayo ikipoteza michezo yake mwili iliyosalia.
Mabao ya Liverpool katika mchezo wa leo yamefungwa na Daniel Sturridge, Philippe Coutinho (mawili) na Divock Origi

HULL CITY YASHUKA DARAJA
Upande wa Hull City, imeshuka daraja rasmi licha ya kusaliwa na mchezo mmoja, hiyo ni baad aya kufungwa mabao 4-0 na Crystal Palace.
Ushindi huo umemaanisha kuwa Palace imefanikiwa kubaki katika Premier League huku Hull City ikiungana na Middlesbrough na Sunderland kushuka daraja.
Mabao yalifungwa na Wilfried Zaha ambaye alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu 2016/17 wa Palace wafungaji wengine ni Christian Benteke, Luka Milivojevic na Patrick van Aanholt.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search