banner

May 29, 2017

MALI YAITWANGA GHANA BAO 1-0 NA KUFANIKIWA KUTETEA TAJI LA UBINGWA AFCON U17

MALI YAITWANGA GHANA BAO 1-0 NA KUFANIKIWA KUTETEA TAJI LA UBINGWA AFCON U17

Timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Mali imeichabanga Ghana kwa bao 1-0 na kufanikiwa kutetea taji la ubingwa michuano ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17 Afrika, (Afcon U17) nchini Gabon.
Baada ya kuingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, Kocha wa Ghana Paa Kwesi Fabin alipanga kikosi chake cha kwanza ambacho kiliifunga Niger 6-5 katika hatua ya penalti kwenye hatua ya nusu fainali.
Ghana walianza kwa kasi kipindi cha kwanza baada ya Eric Ayiah kupata nafasi ya wazi lakini hakuweza kufunga ndipo Momadou Samake akafanikiwa kufunga bao pekee la ushindi.

Kocha wa Ghana, Paa Kwesi Fabin amesema pamoja na kupoteza mchezo huo, wachezaji wake walifanya jitihada za kutosha ila bahati haikuwa upande wake.
Ikumbukwe kuwa Mali  ilikuwa kundi moja na Serengeti Boys na timu hizo zilipokutana katika hatua ya makundi matokeo yalikuwa 0-0.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search