banner

May 20, 2017

SIMBA 2-1 MWADUI FC 'LIVE' FULL TIME, UWANJA WA TAIFA, DAR

SIMBA 2-1 MWADUI FC 'LIVE' FULL TIME, UWANJA WA TAIFA, DAR

FULL TIME
Dakika ya 96: Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba inapata ushindi wa mabao 2-1.
Dakika ya 94: Mwadui ndiyo wanaomiliki mpira na wanasogea katika lango la Simba.
Dakika ya 90: Mwamuzi anaonyesha dakika za nyongeza, mchezo bado kasi yake ni ileile lakini Mwadui wanajipanga kwa kupiga pasi nyingi.
Dakika ya 86: Simba wanapata kona, wanaanzisha kona fupi lakini inakosa faida.
Dakika ya 82: Simba wanalishambulia lango la Mwadui lakini wanakosa ubunifu wa kuwatoka walinzi wa timu hiyo.
Dakika ya 78: Mchezo unaendelea kwa kasi ya kawaida, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika 69: Simba wanafika kwenye lango la Mwadui lakini hakuna madhara yanayotokea.
Dakika ya 65: Simba hawawapi presha kubwa Mwadui ambao wanamiliki mpira na kasi ya mchezo bado haijawa kubwa.
Dakika ya 60: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja.
Dakika ya 55: Mwadui wanamiliki mpira na kuwafanya Simba kupunguza kasi yao katika mchezo huu.
Dakika ya 50: Simba wameanza kipindi hiki lakini kasi yao siyo kubwa kama ilivyokuwa awali.
Mwamuzi anaanzisha kipindi cha pili.
Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.
Tujikumbushe kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo huu wa leo:  Daniel Agyei, Bokungu, Jonas Mkude, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Juuko Murshid,  Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajibu na Juma Luizio.
MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Kipindi cha kwaza kimekamilika
Dakika ya 45: Mchezo unaendelea kwa kasi.
Mwadui wanapata bao la kwanza kupitia kwa Paul Nonga.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 40: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, Mwadui wameanza kuwa makini zaidi na wanawabana Simba katikati ya uwanja.
Dakika ya 32: Kichuya anapata nafasi ya kupiga shuti baada ya kumzunguka beki wa Mwadui lakini shuti lake linapaa juu ya lango.
Dakika ya 30: Simba wanaendelea kulishambulia lango la Mwadui kwa nguvu, pamoja na hivyo wageni nao wanapambana kujipanga lakini wanazidiwa mbinu mara kadhaa.
Ibrahim Ajibu anaipatia Simba bao la pili, ni baada ya kupata pasi nzuri ndani ya eneo la 18, akatuliza mpira na kuutupia wavuni. Simba wana mabao mawili.
Dakika ya 26: Ajibuuuuuuu GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 19: Kichuya anaipatia Simba bao la kwanza kwa njia ya penati, alipiga upande wa kushoto, kipa wa Mwadui, Shaban Kado akaifuata lakini ikawa na kasi kubwa na kuingia ndani.
KICHUYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 16: Simba wanapata penati baada ya Kichuya kuchezewa faulo na kipa wa Mwadui, Shaban Kado wakati akiwa ndani ya eneo la hatari.
Dakika ya 15: Simba wanashambulia lango la Mwadui, Kichuya anapata nafasi ya kupiga shuti anapiga linakuwa na nguvu ndogo na kutoka nje.
Dakika ya 10: Simba wanaendelea kupanga mipango taratibu lakini Mwadui wanakuwa makini.
Dakika ya 5: Bado mchezo haujachangamka.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Saa 10:00: Mwamuzi anaanzisha mchezo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search