banner

May 23, 2017

STAA WA ARSENAL AMNYOOSHEA SHABIKI KIDOLE CHA KATI KISA KUKOSA CHAMPIONS LEAGUE

STAA WA ARSENAL AMNYOOSHEA SHABIKI KIDOLE CHA KATI KISA KUKOSA CHAMPIONS LEAGUE

Arsenal imeshika nafasi ya tano katika Premier League msimu huu uliomalizika, hivyo kukosa ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, jambo ambalo limewakera Wanaarsenal wengi.
Beki wa Arsenal, Hector Bellerin amejikuta akishindwa kuzuia hasira zake baada ya kutanisha na shabiki wa Tottenham kwa kuamua kumyooshea kidole cha kati wakati alipokuwa barabarani.

Kupitia video fupi inayosambaa iliyorekodiwa na shabiki huyo inamuonyesha shabiki akiwa ndani ya gari na kuanza kurekodi video kisha akimdhihaki Bellerin ambaye naye alikuwa kwenye gari lake.

Kuona hivyo, beki huyo akashusha kioo cha gari lake na kuonyesha kidole hicho kisha kuondoka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search