banner

June 10, 2017

BAADA YA KUSHTAKIWA LIVERPOOL YAPOTEZEA DILI LA KUMSAJILI VAN DIJK

BAADA YA KUSHTAKIWA LIVERPOOL YAPOTEZEA DILI LA KUMSAJILI VAN DIJK

Klabu ya Liverpool imeachana na mpango wa kumsajili beki Virgil van Dijk kutoka Southampton.
Liverpool wameamua kuachana na mchezaji huyo baada ya taarifa kuzagaa kuwa walimhadaa beki huyo wa kati kabla hajafanya mazungumzo yoyote na klabu hiyo.

Juzi ilitangazwa kuwa Van Dijk, anakwenda Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 60 (Sh bilioni 135).

Hata hivyo, baada ya taarifa hiyo, Southampton walitoa taarifa kuwa hawajapata ofa yoyote kutoka Liverpool na kuomba bodi ya Premier League kuchunguza kama kuna mazungumzo ya chini yanafanyika.

Saa 24 baada ya ombi hilo ambalo liliridhiwa, Liverpool wametoa taarifa ya kuomba msamaha na kusema kuwa wameachana na dili la mchezaji huyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search