banner

June 10, 2017

MANCHESTER UNITED YAMTEMA IBRAHIMOVIC KISA MAJEREAHA

MANCHESTER UNITED YAMTEMA IBRAHIMOVIC KISA MAJEREAHA

Klabu ya Manchester United imetangaza rasmi kuachana na straika mkongwe Zlatan Ibrahimovic kutokana na kuwa na majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Man United imetangaza kuwa haitamuongezea mkataba mchezaji huyo mara baada ya huu wa sasa kumalizika Juni 30, mwaka huu.

Ibrahimovic alifunga mabao 28 katika msimu wake wa kwanza na kuchangia timu hiyo kupata mataji mawili lakini aliumia goti Aprili 20, mwaka huu katika mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht, inaaminika kuwa anatarajiwa kuwa fiti mapema mwakani ambapo atakuwa na umri wa miaka 36.
Mbali na uamuzi huo lakini Man United imempa ofa mchezaji huyo kuendelea kupatiwa matibabu akiwa klabuni hapo na kama atapona kiasi cha kuwa fiti anaweza kufikiriwa kupewa mkataba mwingine.
o lakini Man United imempa ofa ya kuendelea kupatiwa matibabu akiwa klabuni hapo na kama atapona kiasi cha kuwa fiti anaweza kufikiriwa kupewa mkataba mwingine.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search