banner

July 28, 2017

AJIBU, MANARA NI MWENDO WA KURUSHA MAWE GIZAJI, WAPANOGESHA INSTAGRAM

AJIBU, MANARA NI MWENDO WA KURUSHA MAWE GIZAJI, WAPANOGESHA INSTAGRAM

Wakati msimu wa 2017/18 ukikaribia kuanza, mambo yanaendelea kuwa mazuri huko mitandaoni ambapo sasa vijembe vimekuwa sehemu ya maisha ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Kupitia kurasa za Instagram katika siku za hivi karibuni, watu maarufu katika soka la Tanzania wamekuwa wakiweka maneno ya utani hasa wale wa Simba na Yanga kwa kuwa ni watani wa jadi.
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Ajibu amekuwa kitumia ukurasa wake kuweka maneno ya mafumbo bila kifafanua anamlenga nani, mfano hivi karibuni aliweka picha yake na kuandika: “Ukitaka kujua umuhimu wa ndala ogea raba.”
Japo hajafafanua, lakini inajulikana wazi kuwa Ajibu alitua Yanga akitokea Simba ambao baadhi ya mashabiki na viongozi wa Msimbazi walikuwa wakimpiga madogo juu ya uhamisho wake huo.
Pia kuna posti nyingine, Ajibu ameweka picha yake na kuandika: “I believe Allah in everything I do.”
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara naye hayupo nyuma katika vijembe kuelekea kwa Yanga ambapo moja ya utani alioweka ni kuweka picha ya Msuva na kuandika: “Mungu aibariki miguu yako, kukosa Swaumu yao kwa sasa wasingekuuza, nimeamini njaa haimuachi mtu salama.”
Kauli hiyo ya Manara ni katika utani wake kuonyesha kuwa Yanga hawana fedha ndiyo maana wamekubali kumuuza Msuva kirahisi kwenda nchini Morocco. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search