banner

July 22, 2017

PEP GUARDIOLA ASISITIZA AGUERO HAUZWI

PEP GUARDIOLA ASISITIZA AGUERO HAUZWI

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amethibitisha hana mpango wa kuuza mshambuliaji wake Sergio ‘Kun’ Aguero.
"Ni mchezaji wetu na atabakia hapa," alisema Guardiola wakati akizungumzia tetesi za mchezaji huyo huenda akaondoka.
Hata hivyo kocha huyo amesema wanahitaji kusajili wachezaji wengine watatu au wanne katika kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.
Man City imekua kwenye mawindo ya kuwania saini za walinzi Danilo wa Real Madrid na Benjamin Mendy anayekipiga na katika timu ya Monaco, pamoja na mshambuliaji hatari wa Arsenal Alexis Sanchez.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search