banner

July 01, 2017

VIGOGO WA TFF KUKUTANA LEO KUMCHAGUA KATIBU WA MUDA

VIGOGO WA TFF KUKUTANA LEO KUMCHAGUA KATIBU WA MUDA

Kushikiliwa kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa TTF, Selestine Mwesigwa, ambapo wamesomewa mashitaka 28 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuna maamuzi ya ziada yamefanyika.
Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye pia ni mgombea wa urais katika uchaguzi mguu ujao unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, amesema kuwa Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajiwa kukutana leo Jumamosi kwa ajili ya kumkabidhi majukumu mmoja wa watendaji wa kamati hiyo kukaimu nafasi ya katibu mkuu.

Karia amesema kwa mujibu wa katiba yao, rais anapokosekana kwenye nafasi yake kutokana na sababu yoyote, anayetakiwa kukaimu nafasi yake ni makamu mwenyekiti na kama yeye hayupo basi atateuliwa mjumbe yeyote wa Kamati ya Utendaji mwenye uzoefu ili kuendesha shughuli za kiongozi.

Mwesigwa ndiye mtendaji mkuu katika shughuli za kila siku za TFF, hivyo kukosekana kwake kunaweza kusababisha baadhi ya mambo kutokwenda sawa.  

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search