banner

July 01, 2017

WABISHI WA MWANZA, MBAO FC WAANZA KUJIKUSANYA ILI WAKINUKISHE UPYA

WABISHI WA MWANZA, MBAO FC WAANZA KUJIKUSANYA ILI WAKINUKISHE UPYA

Mbao FC yenye maskani yake wilayani Ilemela jijini Mwanza, baada ya kuonyesha uhodari wa kupambana uwanjani msimu uliopita, sasa wamepanga kuanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara Julai 3, mwaka huu tayari kwa kuingia vitani msimu ujao.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi amesema kuwa, kila kitu kipo tayari kuelekea kambi hiyo.
"Tayari kocha wetu Ettiene Ndayiragije amewasili nchini baada ya kuwa kwenye mapumziko kwao nchini Burundi na kimsingi tumejipanga kuhakikisha kuwa, Mbao inandelea kuwa tishio katika ligi kuu msimu ujao,” alisema Njashi.
Njashi alisema licha ya kuondokewa na nyota wake kadhaa hilo halitawaumiza kichwa bali watapata wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi.
"Sisi kama viongozi tayari tumefanyia kazi ripoti ya mwalimu ambapo yapo baadhi ya mambo alipendekeza yafanyike na sisi tunatekeleza kama yalivyo ili aweze kufanya mipango yake kwa uhuru zaidi kama alivyopanga, hivyo Mbao hatutaki mchezo katika ligi kuu msimu ujao,” alisema kiongozi huyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search