banner

August 21, 2017

AZAM FC YAFANYA MABADILIKO, MENEJA ABDUL SASA NDIYE CEO

AZAM FC YAFANYA MABADILIKO, MENEJA ABDUL SASA NDIYE CEO

Klabu ya Azam imefanya mabadiliko katika uongozi wake hasa katika masuala ya vyeo.
Mabadiliko ya uongozi huo yametangazwa na Ofisa Habari wa klabu hiyom Jaffar Idd Maganga ambapo aliyekuwa meneja wa Azam FC, Abdul Mohamed amepandishwa cheo na kuwa CEO.
Ofisa huyo amesema kuwa Abdul ambaye alikuwa meneja, sasa anakuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo huku Nassor Idrissa aliyekuwa mwenyekiti anapanda na kuingia kwenye bodi ya wakurugenzi wa klabu.
Shani ambaye alikuwa akishika nafasi ya makamu mwenyekiti sasa anakuwa mwenyekiti, naye mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Abdulkarimu anakuwa makamu mwenyekiti. 
Nafasi ya Ofisa Habari imebaki kwa Jaffar Idd huku Simon akiteuliwa kuwa meneja wa timu hiyo.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search