banner

August 21, 2017

KUHUSU TSHABALALA KUIKOSA MECHI YA YANGA, HAYA NDIYO MAJIBU

KUHUSU TSHABALALA KUIKOSA MECHI YA YANGA, HAYA NDIYO MAJIBU

Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye pia anajulikana kwa jina la Zimbwe Jr,
juzi aliumia katika mchezo wa timu yake dhidi ya Gulioni FC, kiasi cha kusababisha hofu kubwa juu ya uwepo wake katika mchezo dhidi ya Yanga.
Tshabalala alicheza mchezo huo kwa mara ya kwanza tangu alipoumia kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC mnamo Mei 27, 2017, tangu hapo alikuwa nje akiwa majeruhi.
Akizungumzia hali ya mchezaji huyo, Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Akifafanua zaidi, Mayanja alisema: “Tshabalala atakuwa vizuri hana tabu yoyote, tunashukuru sana mapokezi ya mashabiki wetu wote wametupokea vizuri naomba waje kwa wingi siku ya Jumatano kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.”
Simba walikuwa Unguja tangu Jumatatu Agosti 14, 2017 kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Yanga.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search