banner

August 20, 2017

SIMBA YAWATANDIKA GULIONI MABAO 5-0, MAVUGO AIBUKA SHUJAA

SIMBA YAWATANDIKA GULIONI MABAO 5-0, MAVUGO AIBUKA SHUJAA

Timu ya Simba, jana usiku ilipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Gulioni FC katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika mchezo huo maalum wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya, Yanga, Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba walitawala mchezo muda mwingi dhidi ya timu hiyo ya Gulioni inayocheza Daraja la Kwanza Zanzibar.
Mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo alifunga mabao mawili dakika za 13 na 40, Shiza Kichuya akafunga dakika ya 37, Juma Luizio dakika ya 41 na Mohammed Ibrahim ‘Mo’ dakika ya 67.
Huo ni mchezo wa pili kwa Simba katika kambi yake ya Unguja kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga, baada ya Alhamisi kulazimishwa sare ya 0-0 na Mlandege ya Ligi Kuu Zanzibar.
Kikosi cha Simba: Aishi Manula/EmManuel Mseja, Erasto Nyoni, Ally Shomary/Mohammed Hussein ‘Thshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali/Paul Bundala, James Kotei/Jonas Mkude, Haruna Niyonzima/Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin/Said Ndemla, Laudit Mavugo/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Juma Luizio na Shiza Kichuya/Jamal Mnyate.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search