banner

August 17, 2017

VIDEO : REAL MADRID YAIFANYA KITU KIBAYA BARCELONA, YABEBA SPANISH SUPER CUP

VIDEO : REAL MADRID YAIFANYA KITU KIBAYA BARCELONA, YABEBA SPANISH SUPER CUP

Timu ya Real Madrid imebeba Kombe la Spanish Super Cup, hiyo ni baada ya kuichapa Barcelona katika mechi zote mbili, ikiwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu imekabidhiwa kombe hilo baada ya kushinda kwa mabao 2-0.
Real Madrid ambayo inafundishwa na Zinedine Zidane ilishinda mechi ya kwanza ugenini kwa mabao 3-1, hivyo kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya Barcelona.
Katika mchezo wa jana usiku, wafungaji wa Real Madrid walikuwa ni Marco Asensio aliyefunga katika dakika ya tatu na Karim Benzema dakika ya 39.
Awali timu hizo zilikutana wiki jana kwenye Uwanja wa Camp Nou, kisha zikarudiana jana kwenye dimba la nyumbani la Madrid ambapo wenyeji walimkosa staa wao, Cristiano Ronaldo aliyefungiwa mechi tano kutokana na kumsukuma mwamuzi, kosa alilolifanya katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo.
 Mchezo huo ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu wa 2017/18 ambazo unazikutanisha timu iliyotwaa ubingwa wa La Liga (Real Madrid) na iliyotwaa ubingwa wa Kombe la Mfalme (Barcelona).
Ushindi huo ni mwanzo mzuri kwa Madrid ambayo pia ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ni mwanzo mbaya kwa Barcelona ambayo imempoteza Neymar hivi karibuni kutokana na mchezaji huyo kusajiliwa na PSG ya Ufaransa.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search