banner

August 30, 2018

BAADA YA KUWATEMA SITA, TFF YAWAPA KITISHO SIMBA

BAADA YA KUWATEMA SITA, TFF YAWAPA KITISHO SIMBA

Na George Mganga

Baada ya kutangaza kuwatema wachezaji sita wa kllabu ya Simba waliokuwa wameitwa katika kikosi cha Taida Stars, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao, amesema hakuna aliye juu ya timu hiyo.

Kidao ameeleza kuwa ukubwa au umaarufu wa jina la mchezaji kupitia klabu yake, haimaanishi kuwa kutakuwa na busara ambayo itaweza kutumika haswa kwa TFF hii ambayo ipo chini ya Wallace Karia.

Katibu huyo amesema Stars inapaswa kupewa heshima yake na nidhamu kuwekwa mbele na ndiyo maana wameamua kuwaondoa wachezaji hao ambao waliitwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018.

Kiongozi huyo amesisitiza kwa kusema nidhamu kwanza ndiyo inapaswa kuwekwa mbele na bila kufuatwa hawatakuwa na cha msalia mtumu kwa kipindi hiki.

Wachezaji walioondolewa ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

Kwa upande wa viongozi wa Simba ambao ni Meneja wa Klabu, Richard Robert ,pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kufuata kanuni limewapeleka kwenye Kamati ya Maadili kwa kutotimiza wajibu wao.


Baada ya kuondolewa, wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao ni Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika na Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search