banner

August 27, 2018

DROO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA ITAPANGWA SIKU YA ALHAMISI HII

DROO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA ITAPANGWA SIKU YA ALHAMISI HII

Klabu nne za England watatambua wapinzani wao katika awamu ya makundi ya mashindano ya kuwania ligi ya mabingwa Ulaya wakati droo itakapofanyika Alhamisi.

Manchester City itakuwa katika chungu cha kwanza na Manchester United na Tottenham Hotspur katika chungu cha pili huku Liverpool ikiwekwa kwenye chungu cha pili au cha tatu.

Droo inatarajiwa kufanyika Grimaldi Forum huko Monaco mwenda wa saa moja usiku saa ya Afrika Mashariki.

Ni vilabu 26 vilivyofuzu moja kwamoja kwa awamu ya makundi, huku sita zikitarajiwa kufuzu baada duru ya pili kukamilika Jumatano.

Uteuzi unafanyikaje?

Washindi katika ligi ya Mabingwa na ligi ya Uropa wanafuzu kuingia katika chungu cha kwanza , pamoja na mabingwa katika mataifa sita yalioorodheshwa juu.

Hii ina maana kuwa kuna timu tatu za Uhispania, miongoni mwa timu kuu msimu huu kwasababu Real Madrid ilishinda kwa mara ya tatu ligi ya Mabingwa, Atletico Madrid nayo ilitawazwa washindii wa taji la ligi ya Uropa na Barcelona ilijinyakulia taji la La Liga.

Vyungu venginevyo hutokana na matokeo ya vilabu vilivyoshindana katika misimu mitano iliyopita kwenye ligi za Ulaya na pia namna ushirikiano wao ulivyokuwa.

Liverpool itafuzu katika chungu cha pili iwapo Benfica haitofuzu, upande ulio na matokeo mazuri katika misimu uiliyopita kuliko wao.

Klabu kimoja kutoka kila chungu kitakutanishwa kuunda makundi manane ya timu nne. Vilabu kutoka taifa moja haviwezi kukutanishwa katika awamu hii.

Zilizopangwa tayari:

Chungu cha kwanza: Real Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester City, Juventus, Paris St-Germain, Lokomotiv Moscow.

Chungu cha pili: Borussia Dortmund, Porto, Manchester United, Shakhtar Donetsk, Napoli, Tottenham Hotspur, Roma.

Chungu cha tatu: Schalke, Lyon, Monaco, CSKA Moscow.

Chungu cha nne: Club Brugge, Galatasaray, Inter Milan, Hoffenheim.

Zinazotarajiwa kuamuliwa: Liverpool, Valencia, Viktoria Plzen, plus six play-off winners.

Matokeo ya awamu ya kwanza ya duru ya pili: Ajax 3-1 Dynamo Kiev, Vidi 1-2 AEK, Young Boys 1-1 Dinamo Zagreb, Benfica 1-1 PAOK, BATE 2-3 PSV, Red Star Belgrade 0-0 Salzburg.

Soka inaanza lini?

Awamu ya kwanza ya makundi katika ligi ya mabingwa Ulaya itachezwa Septemba 18 na 19 huku vilabu vikicheza mechi zao sita za mwisho Desemba 11 au 12 .

Awamu ya mtoano itaanza Februari, huku mashindano yakikamilika kwa fainali katika uwanja wa Atletico Madrid – Wanda Metropolitano Juni mosi, 2019.

CHANZO:BBSSWAHILI

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search