banner

August 30, 2018

POVU JINGINE LAMTOKA MANARA KUHUSIANA NA MASOUD DJUMA

POVU JINGINE LAMTOKA MANARA KUHUSIANA NA MASOUD DJUMA

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kuwa hakuna mtu ambaye atakuwa ndani ya klabu hiyo milele.

Kwa mujibu wa EFM Radio, Manara ameamua kufunguka hayo kutokana na chapisho kuhusiana na taarifa iliyoandikwa Agosti 27 2018 na gazeti la Championi ikieleza kuwa Kocha Msaidizi wa klabu hiyo, Masoud Djuma anaweza akaondoka ndani ya Simba.

Ofisa huyo ameeleza kila aliyepo ameikuta klabu hiyo na akisema viongozi wote waliopo hakuna ambaye ataweza kukaa milele kutokana na kila binadamu anapita hapa duniani.

Chapisho la taarifa hiyo limezidi kumfanya Manara afunguke zaidi huku akiweka msisitizo huo kwa kueleza kuondoka kwa Masoud kunawezekana lakini kwa tartibu maalum.

"Hakuna ambaye atabaki na Simba milele, klabu ya Simba tumeikuta na itaendelea kuwepo, kama wakati wetu wa kuondoka ukishafika watakuja wengine kuendelea nayo" alisema.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search