banner

March 06, 2019

SERENGETI BOYS WAAMKA UTURUKI NA KUITWANGA AUSTRALIA KWA MABAO 3-2

SERENGETI BOYS WAAMKA UTURUKI NA KUITWANGA AUSTRALIA KWA MABAO 3-2

Na Saleh Ally, Antalya

Kikosi cha Serengeti Boys kimeamka na kuitwanga Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya michuano ya Uefa Assist inayoendelea hapa mjini Antalya.

Serengeti Boys ilianza mechi hiyo kwa kusua baada ya kuwaruhusu Australia kutangulia kabla ya kusawazisha katika dakika ya  Edmund John katika dakika ya 16.

Kabla ya kwenda mapumziko, Australia waliandika bao la pili na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili, Serengeti Boys walianza kwa kushambulia kama mbogo hadi walipofanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 81, mfungaji akiwa ni Alphonce John.

Baada ya bao hilo, Serengeti Boys waliongeza mashambulizi na kuonyesha kuwazidi nguvu Australia kabla ya kupata bao la tatu katika dakika ya 89 mfungaji akiwa ni Kelvin John.

Credit : Saleh Jembe blog

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search