banner

May 23, 2019

RATIBA YA FA NI MOTO WA KUOTEA MBALI, LIGI ILIPOTEZA MVUTBAADA YA MECHI 10

RATIBA YA FA NI MOTO WA KUOTEA MBALI, LIGI ILIPOTEZA MVUTBAADA YA MECHI 10

MEI 28 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kufika ukingoni safari ya msimu huu haikuwa salama kwa timu nyingi kutokana na namna ligi ilivyokuwa ikienda yaani ilikuwa bora liende kwa kuwa hamna namna nyingine ya kufanya kwa timu pamoja na viongozi.

Kabla sijaenda mbali niwaambie viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba ratiba ya kombe la mchezo wa kombe la Shirikisho (FA) si rafiki sana kutokana na kuwa karibu na mechi ya mwisho kabla ya msimu.

Ukitazama Lipuli ambayo itacheza mchezo wa fainali Azam FC Juni Mosi mwaka huu, Lindi uwanja wa Ilulu ratiba yake imebana sana.

Jana Jumatano ilicheza na Ndanda FC mkoani Mtwara na ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1, kisha Mei 28 itakuwa Mbeya ikimenyana na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, baada ya hapo siku nne mbele inatakiwa kuwa tena Lindi.

Kwa namna ratiba ilivyo hapo utaona namna ratiba ilivyowabana Lipuli kwani watatakiwa kusairi michezo yake yote huku wakiwa wanafikiria namna ya kushinda michezo itawafanya wasiwe kwenye ubora wao. 

Kwa namna miundombinu yetu ilivyo ni wazi kwamba wachezaji watakuwa wamechoka TFF kwa kina hili kabla ya kuwapa ratiba ya namna hii.

Tukiachana na hili turudi kwenye ligi kuu ambayo kwa sasa ipo hatua ya lala salama na bingwa ameshapatikana tuangalie suala la waamuzi namna ambavyo wamekuwa wakipewa lawama kwa ile michezo inayoonyeshwa moja kwa moja wamekuwa wakitibua na ile ambayo hanyeshwi kumekuwa na madudu.

Mwisho wa siku kila kitu kinakwenda vile ambavyo viongozi wanataka kwani hakuna hatua madhubuti ambazo zimekuwa zikichukuliwa na kama zinachukuliwa ni kwa utaratibu wa kipekee jambo ambalo limekuwa liwavunja moyo wanamichezo.

Tukio moja tu ambalo ninalikumbuka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walifanya uharaka kwenye kutoa maamuzi ni lile la waamuzi waliochezesha mchezo kati ya KMC na Simba lakini kwa mechi nyingine ilikuwa ni lazima kamati ya masaa 72 ikae.

Ni muda sasa wa TFF kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao kuondoa haya matatizo madogomadogo ambayo yanaua kabisa ushindani kwa timu zetu zinazoshiriki ligi kuu pamoja na zile ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza hasa kwa kupitia maamuzi ambayo yanaonekana kama yana ubaguzi.

Kusiwe na maana kwamba mechi ambazo zinafuatiliwa ni zile ambazo timu kongwe kama Simba na Yanga zitacheza basi hatua inakuwa ni mara moja ila kama itakuwa ni Mtibwa, Ruvu Shooting ama Majimaji hawa lazima wasubiri kamati ya masaa 72 haipendezi.

Ushindani unakufa mapema kwenye ligi kama ilivyokuwa msimu huu, mechi 10 za mwanzo zilikuwa bora na ushindani ulikuwa ni mkubwa kwa timu zote kwenye mzunguko wa kwanza, lakini baada ya hapo hakukuwa na ushindani tena kila mmoja akawa anacheza ilimradi anashiriki ligi.

Swali la kujiuliza kwa nini baada ya mechi 10 ushidani uliyeyuka ghafla? Jibu ni moja gharama za kuendesha timu zilikuwa juu na mapato yakawa chini hali iliyofanya timu zianze kupunguza matumizi.

Kama timu zilipunguza matumizi ushindani uliyeyukaje? Baada ya timu kupunguza matumizi hakukuwa na morali kwa wachezaji pamoja na viongozi kuendelea kupambana kwa sababu nguvu yao ilikuwa imefika tamati hawana sehemu ya kupata msaada.

Ngoja niweke sawa kidogo hapo kwenye suala la kuishiwa nguvu na kubana matumizi, msimu huu ligi haikuwa na mdhamini hivyo timu nyingi zilikuwa zinajiendesha kwa kutegemea wadau pamoja na zile fedha ambazo zinatolewa na Azam sasa kutembeza bakuli kwa wadau kulipokata maana yake hata zile posho kwa wachezaji zikakata.

Pia hata gharama za uendeshaji nazo zikazidi kuwa kubwa hali liyofanya wengi kukata tamaa na kushindwa kuendelea kupambana kwa sababu kama timu ilikuwa inaweka kambi wiki moja kabla ya mchezo ilikuwa ni lazima ipunguze aidha wachezaji watoke nyumbani ama wanakutana siku moja kabla ya mchezo.

Tatizo lilianzia hapo yale mazoea ya kuwa pamoja yanapotezwa na sasa kila moja anakuwa na lake kchwani siku ya mechi wachezaji wanakutana tayari ule morali wa ushindani umeshaharibwa kisaikolojia, mchezaji yupo uwanjani ana mambo kama 10 anayafikiria.

Mchezaji anafikiria mshahara wake, matatizo yake ya familia, ugumu wa ligi ulivyo namna mambo ambavyo wanaonewa na waamuzi hali hiyo inakuwa ngumu kwake kucheza kwa kiwango ambacho amekizoea mwisho wa siku tunapata matokeo ambayo kila mmoja anashangaa.

Muda mwafaka kwa TFF kuangalia yale mapungufu yote na kuyafanyia kazi hasa kwa ajili ya msimu ujao ambapo msimu huu tukubali kwamba ligi imepoteza mvuto na hakukuwa na namna nyingine  ya kufanya ilikuwa ni bora liende.




Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search