banner

May 25, 2019

SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA BIASHARA UNITED

SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA BIASHARA UNITED


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa sare waliyoipata leo wanaisahau hesabu zao ni kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Mei 28 uwanja wa Jamhuri.

Simba leo imekubali sare mbele ya Biashara United mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1.

"Tulijipanga kushinda na tumepambana kwa kadri ya uwezo wetu mwisho wa siku tumeambualia sare sio mbaya, tunasahau matokeo tuliyopata, nguvu zetu mchezo wa mwisho.

"Kwa sasa hatupaswi kufikiria mchezo ambao umepita, tunatazama mbele na kujua namna gani tutapata matokeo chanya, mashabiki endeleeni kutupa sapoti," amesema.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search