banner

May 23, 2019

SIMBA, YANGA ZAPEANA TANO, YANGA YAJIPA MATUMAINI MSIMU UJAO

SIMBA, YANGA ZAPEANA TANO, YANGA YAJIPA MATUMAINI MSIMU UJAO


BAADA ya Simba kutetea ubingwa wake msimu huu, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten kuandika ujumbe wa kuwapa pongezi kupitia ukurasa wa Istagram, Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amemjibu kuwa huo ndio uungwana.

Ten aliandika namna hii:- "Hii ni ligi kwa vyovyote lazima mmoja awe bingwa, Hongereni Simba kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

" Machozi miaka zaidi ya mitano mfululizo halikuwa jambo dogo, mlikaa chini mkafikiria na sasa mnafuta machozi yenu.


"Kwetu sisi changamoto za msimu huu zimetufundisha kitu hope tutakuwa bora zaidi msimu ujao," amesema.


Manara wa Simba akajibu namna hii " Dismas ten, tunashukuru sana kwa pongezi zako, huo ni ukomavu mkubwa na hicho ulichokiandika ndio njia ya kufanikiwa.


"Hauhitaji kulalamika lalamika kutwa wakati uhalisia unaujua.


"Nakupa heko na nawaomba wafuasi wenzangu twendeni Ktk page yake tukampe Asante zetu kwa uungwana huu.


"Karibu Taifa leo uone raha ya maisha Simba Sc Vs Sevilla Fc," amesema Manara.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search