banner

June 09, 2019

KOMBE LA FA LILIKUWA NA UGUMU WAKE, SASA NGOMA ISONGE MBELE

KOMBE LA FA LILIKUWA NA UGUMU WAKE, SASA NGOMA ISONGE MBELE


PONGEZI kwa mabingwa wapya wa kombe la Azam Federation Cup (FA) msimu huu ambao ni Azam FC wamepata kile walichostahili licha ya fainali kuwa na changamoto za hapa na pale hizo huwa hazikosekani.

Kila mmoja alikuwa na uhitaji wa kufikia malengo ambayo alijiwekea hivyo kwa hatua ambayo imefika kila mmoja amepata kile alichopanda.

Tumeona changamoto ambazo zilikuwepo hasa kutokana na ugumu wa ratiba kutokuwa rafiki ila mwisho wa siku mchezo umechezwa na bingwa kapatikana hivyo ni muda wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutumia changamoto kama funzo.

Msimu ujao itakuwa bora ratiba ya FA ikiwa rafiki kwa timu zote pia itapendeza uwanja ukiwa ni mmoja kwa ajili ya mashindano jambo litakaloleta hamasa zaidi kwa washiriki kupambana ili kufika hatua ya fainali.

Yote kwa yote nawapongeza wachezaji wa Lipuli FC kwa kupambana na kuonyesha moyo wa kujitoa kwa kweli wanastahili pongezi ingawa hawajabeba kombe kufika hatua ya fainali ni ushindi tosha.

Mashabiki waliojitoa kwa hali na mali wameonyesha njia kwamba watanzania wanapenda mpira ila mpangilio mbovu huwa unawaboa na kuwafanya waishie kwenye vibanda umiza hivyo kuna jambo la msingi linapaswa lifanywe kuboresha mazingira ya soka letu.

Muda wa kujipanga sasa kwa mabingwa ni sasa kwani mashindano yanayofuata ni makubwa zaidi ya haya ambayo mmemaliza hatua ya kimataifa ni kubwa hivyo na maandalizi yake yanapaswa yawe ya kikubwa.

Karibu kwenye jamvi la leo ambapo ningependa kuzungumzia suala zima la mpangilio wa ratiba pamoja na ubora wa miundombinu ya viwanja vyetu kwenye soka la Tanzania.

Kwa sasa tunaona msimu mpya unakuja hivyo TFF wanapaswa wasikae kimya kusubiri mpaka ligi itakapoanza ndipo waanze kutafuta wawekezaji pamoja na kuanza kukagua viwanja.

Kwa yale ambayo yamepita msimu uliopita ni wakati wake kuanza kuyafanyia kazi ili msimu utakaoanza na kila kitu kiende kwa mpangilio mzuri.

Endapo kutakuwa na mpanngilio mzuri ni rahisi kuwavutia wawekezaji kwenye soka letu na kupunguza ile changamoto ya ukata ambao ulikuwa ni wimbo wa klabu zote ambazo hazina udhamini wa kutosha.

Ilikuwa wazi malalamiko yalikuwa ni mengi kuliko shukrani hivyo maana yeke ni kwamba mambo mengi yalikuwa yanakwenda bila mpagilio mzuri ni darasa tosha kwa TFF.

Ukiachilia hilo ilikuwa ni pamoja na suala zima la ratiba namna ilivyokuwa kwenye mpangilio ambao sio rafiki kwa timu nyingi muda wa kuyafanyia kazi hayo yote ni sasa.

Ikumbukwe pia msimu uliopita timu zilikuwa na viporo vingi yote ilitokana na ubovu wa upangaji wa ratiba kuna kitu cha kufanya hapa kabla ya msimu mpya kuanza.

Wengi ambao walikuwa wanacheza viporo walipunguza kabisa morali ya kushindana kutokana na kuanza kupata picha ya timu yao ilipofikia.

Kwa mfano African Lyon waliishiwa nguvu mapema na kupunguza ule ushindani kutokana na kujua kwamba hatma yao inaishia ligi daraja la kwanza msimu mpya hawakuwa na cha kupoteza.

Ikabaki kwa wachache ambao walikuwa wanagombania nafasi za juu pamoja na ubingwa ambao baadaye nako ulikata moja kwa moja na kuwa mbio ya mtu mmoja.

Sasa kama haya yanatokea ni ishara mbaya kwa kuwa hakuna ushindani ligi inapoteza ule mvuto wake na kuwa ya wale wachache wenye manufaa na kile wanachokifanya 
huku wengine wakikata tamaa mapema.

Ili iwe ligi bora kila timu inapaswa ipambane kwa kufanya hiv
yo kutasaidia kupata wachezaji makini watakaofanya kila mmoja avutiwe kutazama michezo yote ya bongo.

Tukigusia kwa upande wa viwanja, ni aibu kuona kwamba ligi kubwa kama ya Tanzania ambayo imekuwa ikukua kila siku viwanja vinakuwa vibovu na timu zinacheza hii haipo sawa.

Ni wakati wa kufanyia maboresho makosa yote yaliyotokea msimu uliopita na kutazama namna mpya ya kuboresha viwanja vyetu viwe bora.

Viwanja vikiwa bora tunapata ladha kamili ya soka na sio kubutuabutua tu mpira ndani inakuwa bora liende, pia hata kupunguza majeruhi inakuwa ni rahisi kuliko hali ya msimu uliopita.

Kuna viwanja vingi sana ambavyo havijawa kwenye ubora wake na vilikuwa vinatumika ni wajibu wa wamiliki kuanza kuviboresha na ikishindkana ni bora vifungiwe kabisa.

Mchezaji anapata raha akiwa anacheza kwenye uwanja bora kama ulivyo wa Taifa hata matokeao unayapata ukiwa na tabasamu ama ukifungwa inakuwa kidogo hauna cha kujitetea kwa upande wa uwanja ni wewe mwenyewe.

Sasa viwanja vingine hakuna hata majani ila wachezaji wanaingia kucheza, tena ni ligi kuu ujue inarudisha nyuma maendeleo ya soka letu ni lazima tuwekeze kwenye kila idara kuwa bora.

Tukiwa na ligi bora itawavutia wawekezaji kupena kuwa sehemu ya ligi yetu jambo ambalo litapunguza ule ugumu wa uendeshaji kwenye ligi yetu.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search