banner

October 14, 2019

FULL TIME: MASHUJAA 0-1 SIMBA SC, MECHI YA KIRAFIKI

FULL TIME: MASHUJAA 0-1 SIMBA SC, MECHI YA KIRAFIKI


FULL TIME; MASHUJAA FC 0-1 SIMBA SC

Dak ya 90, dakika tatu zimeongezwa.
Dak ya 85, hatari nyingine inatokea katika lango la Simba, kipa Manula anadaka mpira na kulala kwa madaha.

Dak ya 79, Kona inapigwa kuelekea lango la Mashujaa, imepigwa chinichini japo inakosa macho, inaokolewa.
Dak ya 75, nafasi nyingine Simba wanakosa nafasi ya wazi, inakuwa faida kwa Mashujaa.
Dak ya 70, imepigwa pale na Manula anadaka kiulaini.
Dak ya 69, Ndemla anacheza madhambi na anaonyeshwa kadi ya njano, ni eneo zuri pale kwa Mashujaa kusawazisha bao.
Dak ya 65, Ndemla anapiga mashine moja kali, inapaa juu ya lango.

Dak ya 56, Shiboub anaifungia Simba bao la kwanza, sasa ni 1-0.
Dak ya 53, Rashid Juma anajaribu shuti moja ambalo linakuwa mkaa.
Dak ya 46, Mlipili anatuliza mpira, piga mbele na Mashujaa wanaokoa na kutoa nje, sasa unarushwa kwenda kwao.
Dak ya 46, utulivu kwa timu zote mbili haujaonekana, inawezekana sababu ya uwanja kutokuwa vizuri.
Dakika 45 za kipindi cha pili zimeanza

HALF TIME: MASHUJAA 0-0 SIMBA SC

Dak ya 45, zimeongezwa dakika mbili, na sasa kona inapigwa kuelekezwa Simba, tayari imeshapigwa na Manula anaokoa, anarusha mpira mbele.
Dak ya 43, Kona kuelekea lango la Mashujaa, anapiga Kahata na inaokolewa.
Dak ya 41, faulo inapigwa kuelekezwa Mashujaa, anaonekana Ndemla yupo na mpira. Piga paleee, inagonga mwamba na kutoka nje.
Dak ya 40, Simba wanajaribu kila namna ya kuwatoka mabeki wa Mashujaa lakini inakuwa ngumu, wamewadhibiti vilivyo.
Dak ya 36, Ndemla anajaribu kuipenya ngome ya Mashujaa, inashindikana, sasa unamkuta Rashid Juma, unatoka nje na Mashujaa wanarusha.

Dak ya 34, Manula anaanza upya, baada ya mpira kuwa golikiki.
Dak ya 30, Ni kona kwa Simba, inapigwa lakini inakosa mmaliziaji, Mashujaa wanapanda na mpira.
Dak ya 29, Si goli, Mwamuzi anasema kuna madhambi yalifanyika kabla ya kufungwa, sasa Mashujaa wanaanza upya.
Dak ya 27, Simba wanapachika bao lakini Mwamuzi wa pembeni ananyoosha kibendera juu.
Dak ya 22, Mashujaa wanafanya shambulizi lingine la hatari, inakuwa kona, inapigwa pale lakini wanaokoa mabeki wa Simba.

Dak ya 21, Mashujaa wanapata kona ya kwanza, ni ya kwanza kwa mchezo huu, pigwa pale, inakuwa golikiki.
Dak ya 16, dimba la Tanganyika limekuwa na changamoto kwa wachezaji wa Simba, mipira yao haitulii.
Dak ya 11, Simba wanafanya shambulizi moja zuri, kilichotokea ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri.
Dak ya 9, Mpira umetoka sasa, Simba wanarusha kuelekea lango la Mashujaa.
Dak ya 8, tayari mechi imeshaanza katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search