banner

October 13, 2019

MBABE: SASA NITAMNYOOSHA KILA ATAKAYEKATIZA ANGA ZANGU

MBABE: SASA NITAMNYOOSHA KILA ATAKAYEKATIZA ANGA ZANGU



ABDALAH Panzi ‘Dulla Mbabe’ Bingwa wa  ubingwa wa Shirikisho la Ngumi za kulipwa Duniani (WBO) Asia Pacific uzito wa kati (Super Middle) ambao aliupata hivi karibuni kwa kumtwanga Zulipikaer Maimaitiali raia wa China amesema kuwa kwa sasa atamchapa kila anayekuja mbele yake.

Ushindi huo ambao umempa heshima Mbabe ulimpa fursa ya kupeleka mkanda huo bungeni aliupata kwa kumnyoosha mpinnzani wake kwa TK raundi ya tatu umeipandisha chati Tanzania kwa upande wa ngumi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mbabe amesema kuwa ana imani na kile ambacho anakifanya kutokana na maandalizi ambayo anayafanya jambo linalompa matumaini kuwafundisha adabu mabondia watakaohitaji kupambana naye.

“Mchina amenijenga na kunipa uwezo mkubwa wa kujiamini na kuona kwamba nami pia nina uwezo wa kupeperusha bendera ya Taifa kimataifa, kazi yangu kwa sasa kila atakayejichanganya kwenye anga zangu ni lazima nitamyoosha bila kuogopa,” amesema Mbabe.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search