banner

November 16, 2019

TAIFA STARS YAKWEA PIPA KUWAFUATA LIBYA, MMOJA AACHWA BONGO

TAIFA STARS YAKWEA PIPA KUWAFUATA LIBYA, MMOJA AACHWA BONGO


TIMU ya Taifa ya Tanzania leo imekwea pipa kuwafuata wapinzani wao Libya mchezo wao wa pili wa kufuzu michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyka nchini Cameroon 2021.

Sars itamenyana na Libya nchini Tunisia ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea mchezo uliochezwa jana uwanja wa Taifa.

Kwenye msafara huo nyota Erasto Nyoni ambaye ni kiraka ameachwa Bongo akipata matibabu ya goti.

Etienne Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa ameachwa Nyoni kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata jana kwenye mchezo dhidi ya Equatorial Guinea.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search