banner

February 20, 2020

BAADA YA KUIBANA YANGA, POLISI TANZANIA YATAJA KINACHOWABEBA

BAADA YA KUIBANA YANGA, POLISI TANZANIA YATAJA KINACHOWABEBA

MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania aliyetoka kuwabana Yanga kwa kugawana pointi mojamoja Uwanja wa Ushirika amesema kuwa uwezo wa vijana wake uwanjani unatokana na kutambua majukumu yao kwa ufasaha jambo linalowafanya wajitume.

Polisi Tanzania yenye maskani yake Moshi inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumamosi, Uwanja wa Ushirika dhidi ya Ruvu Shooting.

Hamsini amesema:"Wamekuwa makini kuskiliza maagizo ambayo wanapewa licha ya wakati mwingine kushindwa kufanya ipasavyo ila ni sehemu ya mchezo kwani kukosea ni kawaida.

"Kwa namna ambavyo ninawaona nina imani tutaendelea kupata matokeo mazuri kikubwa ni sapoti kwa mashabiki kwa ajili ya kuishangilia timu yao," amesema.

Mchezo uliopita Polisi Tanzania ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga itamenyana na Ruvu ambayo imetoka kushinda mabao 2-1 mbele ya Coastal Union.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search