banner

February 14, 2020

LIPULI:NJOONI SAMORA MPATE BURUDANI

LIPULI:NJOONI SAMORA MPATE BURUDANI



UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho, Februari 15, Uwanja wa Samora kuona watakachomfanya mnyama Simba bila  mashaka.

Lipuli inakumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 4-0 nahodha wao Paul Nonga na Daruesh Saliboko wote wametupia jumla ya mabao nanenane.

Akizungumza na Saleh Jembe , Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa maandalizi yapo vizuri ni suala la muda kupata pointi tatu Samora.

"Mchezo wa kwanza tulifungwa hilo tunalitambua na benchi la ufundi limefanyia kazi makosa yaliyopita ila mchezo wetu wa Jumamosi watatusamehe, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuujaza Uwanja wa Samora kushuhudia namna tutakavyofanya mbele ya mnyama.

"Mwalimu yeye anaendelea na kuwapa mbinu wachezaji na kuhusu namna tutakavyowamaliza wapinzani wetu kwa sasa hatuwezi kusema mambo yote yatakuwa uwanjani kikubwa sapoti na tunajiamini katika hili," amesema Sanga.

Lipuli ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 29 huku Simba ipo nafasi ya Kwanza na pointi 53 kibindoni.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search