banner

February 25, 2020

SIMBA YAMYOOSHEA MIKONO LUIS

SIMBA YAMYOOSHEA MIKONO LUIS


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa kasi ya kiungo mshambuliaji wao, Luis Miquissone haipaswi kupuuzwa kwani anaonyesha vitu vya kipekee ndani ya timu hiyo.

Luis ametupia bao moja ndani ya Klabu ya Simba na pasi moja ya bao mbele ya Biashara United baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea UD Songo amekuwa akionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi anazopewa nafasi.

Bocco amesema:-"Yupo vizuri hasa kwa namna anavyopambana na kuonyesha kile alichonacho ndani ya uwanja na tukiwa kwenye mazoezi pia kuna vitu vya kipekee anavyovionyesha ni matumaini yetu kwamba ataonyesha mengi zaidi.

"Kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye ligi na mashindano mengine ambayo tutashiriki ila kasi ya Luis siyo ya kupuuza kwani anaonyeha uwezo mkubwa,".



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search