banner

April 07, 2020

MANCHESTER CITY YAMLILIA MAMA WA PEP GURDIOLA ALIYEFARIKI KWA CORONA

MANCHESTER CITY YAMLILIA MAMA WA PEP GURDIOLA ALIYEFARIKI KWA CORONA


UONGOZI wa Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu England umethibitisha kutokea kifo cha mama mzazi wa Kocha Mkuu Pep Guardiola aliyefariki jana kwa Virusi vya Corona.
Dolors Sala Carrio ametangulia mbele za haki akiwa na umri wa miaka 82 akiwa Manresa, Barcelona.
Taarifa za kifo chake zinatokea wiki moja baada ya Guardiola kutoa msaada kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Wachezaji na viongozi wamesema kuwa wapo pamoja na kocha huyo kwenye kipindi hiki kigumu ambapo wengi wametumia mitandao yao ya kijamii kumpa pole kwa pigo alilolipata.
Kevin de Bruyne kiungo mshambuliaji wa City amesema kuwa wao ni familia moja na ni timu moja.
"Mawazo yetu kwa sasa yapo kwenye familia ya Pep na familia yake kiujumla, sisi ni timu moja.
Raheem Sterling amesema ," Maombi yangu yote na mawazo yangu ni juu ya familia ya Pep kwa wakati huu mgumu.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search