banner

April 05, 2020

TIMU TATU KUBWA ZAINGIA VITANI KUIWINDA SAINI YA MARIO GOTZE WA DORTMUND

TIMU TATU KUBWA ZAINGIA VITANI KUIWINDA SAINI YA MARIO GOTZE WA DORTMUND



MARIO Gotze, kiungo anayekipiga ndani ya Borussia Dortmund saini yake imegeuka lulu kwa kuwaniwa na klabu kubwa ambazo zinahitaji huduma yake ikiwa ni pamoja na West Ham United, Everton na Roma.
Matumaini ya klabu hizo ni kuipata saini ya nyota huyo bure kwani mkataba wake unameguka Juni 30 msimu huu huku ikielezwa kuwa hana mpango wa kusaini dili jipya.
Akiwa ndani ya Dortmund kiungo huyo mwenye miaka 27 amecheza mechi 13 na kutupia mabao matatu msimu huu, huku kabu yake ikiwa kwenye mwendelezo wa kumshawishi abaki ndani ya klabu hiyo.
Roma ambayo inayoshiriki Serie A ipo kwenye vita na timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni Everton na West Ham, zote zinahitaji kupata huduma yake.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search